Nyota wa muziki nchini Bahati ametunukiwa tuzo ya silver Plaque na mtandao wa kupakua na kusikiliza muziki wa boomplay Kenya.
Hii ni baada hitmaker huyo wa “Pete yangu” kufikisha zaidi ya streams millioni 8 kupitia nyimbo zake zote zilizopakiwa kwenye mtandao huo.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram bahati amewashukuru mashabiki zake kwa kuendelea kufuatilia kazi zake ambazo zinazidi kuonyesha mafanikio makubwa ndani na nje ya Kenya.
Tuzo hizo maarufu kama ‘Boomplay Plaques’ hutolewa kutambua jitihada za wasanii wanaofanya vizuri kwenye App ya Boomplay.