You are currently viewing 2 Chainz aonyesha pesa alizoficha Marehemu Baba yake

2 Chainz aonyesha pesa alizoficha Marehemu Baba yake

Rapa kutoka nchini Marekani 2 Chainz ameonyesha pesa nyingi ambazo baba yake aliyefariki zaidi ya miaka kumi iliyopita aliziacha bila taarifa kwenye nyumba ya rapa huyo.

Kupitia Ukurasa wake wa Instagram 2 Chainz ameweka video kwenye Instastory inayoonyesha fedha hizo ambazo nyingi zimekunjwa huku akisikika akisema ‘Nilikuwa na tafrija kwa ajili ya siku yangu ya kuzaliwa nyumbani siku iliyofuata nikawa naweka vizuri nyumba nikakuta pesa hizi ambazo baba yangu aliziacha kwenye Basement,pumzika kwa amani baba’.

Baba mzazi wa 2 Chainz alifariki dunia mwezi Julai mwaka 2012 ikiwa ni wiki chache kabla ya rapa huyo kuachia album yake ya ‘Based On A T.R.U Story’.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke