You are currently viewing 20 PERCENT AMJIBU HARMONIZE

20 PERCENT AMJIBU HARMONIZE

Hatimaye ahadi ya Harmonize ya kuingia studio na kufanya kolabo na 20 percent pindi tu akitua Tanzania kutoka nchini Marekani imepokelewa kwa mikono miwili na mkali huyo wa zamani.

20 Percent ametumia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram kumjibu Harmonize kuwa “Promise is like a debt”  kwa maana yupo tayari hivyo Harmonize atimize alichokiahidi.

20 percent ambaye ni mshindi wa tuzo tano za Kili Music Awards mwaka wa 2010, aliwahi kutamba na ngoma kama Maisha ya Bongo, Mama Neema, Money Money, Tamaa Mbaya na nyingine kibao.

Haya yanajiri baada ya usiku wa kuamkia Oktoba 25 kuwa mrefu sana kwa harmonize ambaye alionekana akiburudika na midundo ya 20 Percent na kupelekea kutoa ahadi ya kufanya nae kolabo, sambamba na kueleza kuwa ni ndoto yake ya muda mrefu.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke