You are currently viewing 50 cent adai Eminem hapewi heshima anayostahili

50 cent adai Eminem hapewi heshima anayostahili

Rapa mkongwe kutoka nchini Marekani 50 Cent amesema rapa Eminem hapewi heshima ya kutosha. Kwenye mahojiano yake na ‘Ebro In The Morning’ wakati akiitangaza series yake mpya (Hip Hop Homicides), 50 Cent amesema kwa mchango ambao Eminem ameuweka kwenye huu muziki wa Hiphop, anafikiri anastahili heshima zaidi ya ambayo anapewa kwa sasa.

Ikumbukwe ‘Eminem’ ndiye rapa mwenye rekodi nyingi za mauzo yaani Most Certified Artist katika historia ya muziki nchini Marekani, mpaka sasa ana jumla ya certificate Million 73.5 kwa upande wa Gold & Platinums.

Eminem anashikilia rekodi ya msanii aliyeuza singo nyingi zaidi katika kiwango cha (Gold) na (Platinum) yaani mauzo kuanzia nakala laki tano hadi milioni moja, akishika namba moja katika historia ya RIAA Awards.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke