You are currently viewing 50 CENT AMTOLEA UVIVU JAY Z KWA MADAI YA KUTOMTAKA KWENYE SUPER BOWL HALF TIME SHOW

50 CENT AMTOLEA UVIVU JAY Z KWA MADAI YA KUTOMTAKA KWENYE SUPER BOWL HALF TIME SHOW

Rapa kutoka Marekani Jay-Z hakutaka 50 Cent atumbuize kwenye Halftime show ya Super Bowl 2022, ilimbidi Eminem atie mgomo kwa kusema hatofanya show kama Jay-Z hatomruhusu 50 Cent awe kwenye orodha ya watumbuizaji kwenye fainali hizo.

Siri hii imevujishwa na Mtangazaji N.O.R.E kwenye podcast ya Drink Champs wakati akifanya mahojiano na Snoop Dogg.

Kauli hiyo ilimuibua 50 Cent jana kwenye akaunti zake za mitandao ya Kijamii ambapo alimshutumu vikali Jay-Z kwa kuiga mtindo wa nywele wa mchoraji maarufu duniani Jean-Michel Basquiat huku akimkejeli kwa kumuita shoga.

“Kwa nini alilazimika kusema hilo liwe swali? NORE Mke wako mkubwa anakimbia huku na huko akijaribu kuonekana kama mchoraji shoga,” 50 Cent alifoka.

50 hakuishia hapo. Rapper huyo alipinga madai ya Noreaga kwamba Jay-Z alimwita Eminem “mzungu.” Kwa kusema kwamba “Kwanini alisema yule kijana wa kizungu, kwanini hangesema msanii mkubwa wa rap duniani? Pasaka njema ! mtu kufurahia likizo. @bransoncognac @lecheminduroi,” 50 Cent alihitimisha kupitia Instagram yake.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke