You are currently viewing 50 CENT ATANGAZA KUSTAAFU MUZIKI MARA BAADA YA KUACHIA ALBUM YAKE MPYA

50 CENT ATANGAZA KUSTAAFU MUZIKI MARA BAADA YA KUACHIA ALBUM YAKE MPYA

Nguli wa muziki wa hiphop kutoka nchini Marekani 50 Cent  ametangaza kuacha muziki mara baada tu atakapoachia album yake mpya ambayo ana mpango wa kuiachia hivi karibuni.

Kupitia ukurasa wake wa instagram rapa huyo ambaye amekuwa game ya muziki wa Hiphop kwa miaka 14 amesema amekuwa kwenye game ya muziki kwa muda mrefu na sasa ni wakati wake wa kupumzika na kuacha wasanii wengine waendelee.

 “Smile my next album might be the my last terrorized hiphop for 14 years”ameandika 50 Cent kwenye Instagram yake.

Taarifa 50 Cent kustaafu muziki imewaacha mashabiki zake na mshangao kwani wengi wamekuwa na kiu ya muziki wake baada ya kuachia album yake ya  Animal Ambition ya mwaka wa 2014.

Ikumbukwe wasanii wengi nchini marekani wamekuwa wakitangaza kuacha muziki lakini mwisho wa siku wanarejea tena kwenye muziki ingawa baadhi ya mashabiki wa muziki duniani wanahisi huenda keysha cole tayari amefanya ya kustaafu muziki.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke