Mwaka 1993 wakati Snoop Dogg akirekodi album yake ‘Doggystyle’ alikumbana na kesi ya mauaji kufuatia Kifo cha member wa kundi hasimu ambapo ilidaiwa aliuawa kwa kupigwa risasi na bodyguard wa Snoop Dogg.
Album hiyo ya Snoop Dogg ilienda sambamba na usikilizwaji wa kesi yake kiasi cha kupelekea mauzo ya album hiyo kupaa juu na kutengeneza historia kufuatia pia wimbo ‘Murder Was the Case’ uliokuwemo kwenye album hiyo.
50 Cent akiwa kama mtayarishaji mkuu ametangaza ujio wa series iitwayo ‘Murder Was the Case’ chini ya STARZ akishirikiana na rapa Snoop Dogg ambapo itaangazia kisa chote cha tukio hilo ambalo lilimuweka Snoop chini ya ulinzi hadi February 20, 1996 alipoachiwa huru.