You are currently viewing 50 CENT KUJA NA FILAMU ITAKAYOANGAZIA MAUJI YA MARAPA NCHINI MAREKANI

50 CENT KUJA NA FILAMU ITAKAYOANGAZIA MAUJI YA MARAPA NCHINI MAREKANI

Nyota wa muziki wa kutoka Marekani 50 Cent ambaye kwa sasa amejikita zaidi kwenye uandaaji wa Filamu na uigizaji ametangaza kuachia tamthia itakayoonesha Kesi za mauaji ya Rapa mbalimbali ambazo zimeshindwa kupatiwa ufumbuzi.

50 anaandaa tamthilia hiyo kwa kushirikiana na Mona Scott-Young Monami na Lionsgate. Tamthilia hiyo itaongozwa na Van Lathan ambaye ni mshindi wa tuzo ya Oscar kupitia kipengele cha muongozaji bora wa Filamu fupi ya Two Distant Strangers.

Tamthia hiyo itaitwa Hiphop Homicides na 50 Cent anataka kuonesha mambo yote maovu ambayo hupelekea mauaji ya wasanii wa HipHop ambayo yanarindima kila siku nchini Marekani.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke