You are currently viewing 50 Cent mbioni kuja na filamu kuhusubmaisha ya tapeli maarufu wa Nigeria, Hushpuppi

50 Cent mbioni kuja na filamu kuhusubmaisha ya tapeli maarufu wa Nigeria, Hushpuppi

Rapa, muigizaji na muandaaji wa show za Tv na filamu kutoka Marekani, Curtis James Jackson III maarufu kama 50 Cent, ametangaza mpango wake kwa mashabiki kwamba anaandaa series itakayohusu maisha ya Ramon Abbas maarufu Hushpuppi ambaye ni raia wa Nigeria aliyejipatia umaarufu mkubwa duniani kwa utapeli mitandaoni.

50 Cent ambaye ameshatayarisha series kama Power, Power Book II, Power Book III: Raising Kanan ameeleza kupitia ukurasa wake wa Instagram kuhusu ujio wa series ya Hushpuppi na kusema ni hivi karibuni.

“Kwa walaghai wangu nilipaswa kufanya hivi, tamthilia kumuhusu Hushpuppy inakuja hivi karibuni” – Unasomeka ujumbe wa 50 Cent kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Hushpuppi ambaye wiki iliyopita alihukumiwa kifungo cha miaka 11 gerezani, hata hivyo kulingana na tayari alishakaa jela Marekani kwa takribani miaka 2 tangu mwezi Juni mwaka 2020 baada ya kukamatwa huko Dubai na kisha kuhamishiwa Marekani, hivyo kwasasa ameanza kukitumikia kifungo chake cha miaka 9 tu gerezani.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke