Mkongwe wa muziki wa Hiphop kutoka Marekani 50 Cent ameuweka muziki kando, anaendelea kujikita kwenye upande wa kutayarisha filamu na vipindi vya televisheni. Siku chache baada ya kutangaza kuja na series ‘Murder Was the Case’ ambayo itagusia historia ya kweli ya rapa Snoop Dogg, 50 Cent ametangaza tena ujio wa series mpya nyingine chini ya Starz.
Kupitia ukurasa wake wa instagram, 50 Cent alitudokeza kuhusu ujio wa series iitwayo ‘Queen Nzinga’ ambayo itaangazia na kujikita kwenye maisha ya malkia huyo wa Kiafrika katika Karne 17 nchini Angola.
Uhusika mkuu utavaliwa na Yetide Badaki ambaye pia ni mtayarishaji mkuu series hiyo.