You are currently viewing A PASS AKERWA NA WASANII WANAOHONGA VYOMBO VYA HABARI UGANDA KUCHEZA NYIMBO ZAO

A PASS AKERWA NA WASANII WANAOHONGA VYOMBO VYA HABARI UGANDA KUCHEZA NYIMBO ZAO

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda A Pass hajafurahishwa na tabia ya watu ambao wamekuwa na mazoea ya kuzilipa vyombo vya habari kucheza muziki wao.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, A Pass amewaomba wanahabari kuacha suala la kuchukua pesa kutoka kwa mameneja wa wasanii ili kucheza muziki wao hewani.

Anasema kuwa kitendo cha kulipa vyombo vya habari kucheza muziki mbovu kumesababisha kusaulika kwa wasanii wenye vipaji ambao hawana pesa za kuhonga.

Aidha ameeleza kuwa njia inayotumika kuwatangaza wasanii wasiokuwa na vipaji inazidi kuleta madhara kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda badala ya kuleta maendeleo.

A Pass pia amebainisha kuwa kuna wasanii wengi wenye vipaji ambao wanataka kukuza muziki wao lakini wanashindwa kutokana na kizingiti ambacho kimewekwa na wale wanaolipa wanahabari.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke