Mrembo mwenye kipaji kikubwa, Abby Chams ambaye amesaini mkataba na kampuni ya Sony Music Entertainment, amesema anajivunia kujiunga na lebo hiyo kubwa ya muziki kwani ndoto zake zinakwenda kutimia haraka.
Akizungumza mara baada ya kusaini dili hilo Juni 8, 2022, Abigial amesema anajiona mwenye bahati na anaahidi kufanya makubwa kwani kazi yake inakwenda kuwa nyepesi chini ya Sony.
“Najiona mwenye bahati ya kipekee kuwa mmoja wanafamilia wa lebo kubwa Afrika, ndoto zangu zimetimia, Ninaahidi kuwapa mashabiki wangu vitu vizuri zaidi,” alisema.
Kwa upande wake mkuu wa Sony Music Afrika Mashariki, Christine ‘Seven’ Mosha, amesema anafahamu uwezo wa binti huyo mwenye sauti nzuri ya kuvutia mashabiki hivyo anafurahi kuwa naye.
Mrembo huyo anatarajia kuachia wimbo wake mpya wa U and I Ijumaa hii, Juni 17.