You are currently viewing ABBY CHAMS ADAI CHANGAMOTO YA KUTONGOZWA NA MAPRODYUZA KARIBU IMFANYE AACHE MUZIKI

ABBY CHAMS ADAI CHANGAMOTO YA KUTONGOZWA NA MAPRODYUZA KARIBU IMFANYE AACHE MUZIKI

Msanii wa Bongofleva, Abby Chams anasema amepitia changamoto katika harakati zake kama msanii wa kike hasa katika mchakato wa uandishi wa muziki, kurekodi na kuhakikisha kwamba wimbo wake unasikizwa na umma.

Abby anasema kwamba kwa miaka mingi tangu aanze safari ya muziki amekabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kutongozwa na watayarishaji wa muziki na waelekezi wa video.

“Ukweli mimi kama mwanamuziki kwenye sekta hii zipo changamoto, unajua nina miaka 18 tu na unajua ninafanya kazi na watu wengi, Producers na Directors ni wakubwa sana kwangu- ni kama wazee, wananitongoza, Yaani wananiweka kwenye hali ambayo sio nzuri “, anasema.

Msanii huyo ameiambia BBC kwamba tabia hiyo ilimkera sana hadi kulazimika kukataa uhusiano wa kibiashara na baadhi ya watu aliokuwa akifahamiana nao.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke