Mwimbaji mpya wa bongo fleva Abby Champz ameendelea kupiga hatua kwenye muziki wake.
Mrembo huyo ametumbuiza kwenye maonesho ya kibiashara ya Umoja wa Falme za Kiarabu, Expo 2021 Dubai ambayo yalizinduliwa Oktoba 1 mwaka huu.
Maonesho hayo ya kimataifa yamekuwepo katika aina mbalimbali kwa zaidi ya karne mbili, kama fursa kwa mataifa kuonyesha teknolojia mpya, bidhaa na maoni.
Abby Chams ambaye anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Tucheze’ amekuwa na muendelezo mzuri wa rekodi kwenye muziki wake kwani mwezi uliopita alionekana kwenye kipindi maarufu cha televisheni nchini Marekani ‘The Kelly Clarkson Show’