Msanii wa muziki nchini Adasa amezua gumzo mtandaoni baada ya kufunguka kuwa amekuwa akipitia kipindi kigumu maishani mwake.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook mrembo huyo ameweka wazi kuwa hivi karibuni maisha yamekuwa yakimlemea japo tumaini lake bado liko kwa Mungu.
Hata hivyo licha ya kutoeleza ni nini hasa kinachomsibu maishani, mashabiki zake wameonekana kumfariji kwa kumtumia jumbe za kumtia moyo.