Adele ni miongoni mwa wasanii wenye nguvu sana upande majukwaa ya kusikiliza muziki mtandaoni hasa mtandao wa Spotify. Sasa nguvu yake imepelekea mtandao huo kuondoa kipengele cha ‘Shuffle’ ambacho kilikuwepo upande wa kusikiliza album.
Mtumiaji wa mtandao huo alikuwa hawezi kusikiliza nyimbo zilizopo kwenye album kwa mtiririko wa namba kama zilivyopangwa kwenye Tracklist. Kufuatia ombi ambalo alilifanya baada ya kuachia album yake mpya ’30’ Spotify wamekubali kuondoa kitufe hicho.