You are currently viewing ADELE AMWAGA MACHOZI AKITANGAZA KUAHIRISHA MATAMASHA YAKE YA MJINI LAS VEGAS

ADELE AMWAGA MACHOZI AKITANGAZA KUAHIRISHA MATAMASHA YAKE YA MJINI LAS VEGAS

Mwanamuziki kutoka Uingereza Adele amejikuta akimwaga machozi wakati akitangaza kuahirishwa kwa maonesho yake 24 ya mjini Las Vegas (Las Vegas Residency) ambapo onesho la kwanza lilipangwa kuanza Januari 21 mwaka huu katika ukumbi wa Caesars Palace’s Colosseum.

Adele amesema kuahirishwa kwa maonesho yake kumekuja kufuatia nusu ya timu yake kukutwa na maambukizi ya Corona.

“Naomba msamaha, tamasha langu haliko tayari. Nusu ya Wafanyakazi wangu wana maambukizi ya corona hivyo basi imekuwa vigumu kumaliza maandalizi ya tamasha hilo.” alizungumza Adele kwenye video ambayo alichapisha kwenye mitandao ya kijamii.

Tangazo la maonesho hayo lililotolewa mwezi Novemba, lilisema kwamba mwimbaji huyo wa Uingereza atakuwa akifanya maonesho mawili kila wikendi hadi mwezi April 2022. Tiketi ziliuzwa kati ya $85 hadi $685, na Adele alitarajiwa kujipatia zaidi ya (£500,000) kwa kila onesho ambazo ni zaidi ya shillingi millioni 56.8 za Kenya

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke