Kampuni ya mitindo na mavazi Adidas imetangaza kuendelea kuuza bidhaa za rapa Kanye West “Yeezy” bila kutumia jina hilo.
Siku ya jana kampuni hio ilitangaza kuachana rasmi na rapa huyo, baada ya kauli zake za chuki dhidi ya watu wa jamii ya kiyahudi.
“Bidhaa zote za Yeezy zitauzwa chini ya jina la Adidas na zitatambulika kama bidhaa za Adidas” – Chanzo kutokea Adidas.
Kampuni ya Adidas imeripotiwa kuwa itapoteza takribani shillingi millioni 30 mwaka huu kufuatia kuvunja uhusiano wake Kibiashara na Kanye West.