You are currently viewing Adidas yathibitisha Ronaldo hakugusa mpira kwenye mchezo wa Ureno dhidi ya Uruguay

Adidas yathibitisha Ronaldo hakugusa mpira kwenye mchezo wa Ureno dhidi ya Uruguay

Kampuni ya Adidas ametoa majibu ya utata wa Cristiano Ronaldo kwamba aliugusa au hakuugusa mpira ambao uliingia golini na Bruno Fernandes kutajwa kama mfungaji wa bao hilo kwenye mchezo wa Ureno dhidi ya Uruguay.

Adidas wamesema Ronaldo hakuugusa mpira huo, Asante kwa kifaa maalum cha kuhisi (sensor) kilichopachikwa kwenye mpira huo unaotumika kwenye michuano hiyo ya Kombe la Dunia mwaka huu nchini Qatar.

Timu ya Taifa ya Ureno imejihakikishia nafasi kwenye hatua ya 16 bora baada ya kupata ushindi wa 2-0 dhidi Uruguay kwenye mchezo wa kundi H

Ureno inaongoza kwenye msimamo wa kundi H ikiwa imefikisha alama 6.

Michezo ya mwisho itaamua timu itakayoungana na Ureno kwenye hatua ya mtoano katika kundi hilo lenye timu za Ghana na South Korea.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke