Akaunti ya YouTube ya mwanamuziki wa Bongofleva Diamond Platnumz imefutwa na wamiliki wa YouTube kwa kile kinachoelezwa kwamba imekiuka miongozo ya mtandao huo.
Ukiingia kwenye Akaunti hiyo kwa sasa, kuna ujumbe unasema ‘akaunti hii imefutwa kwa kukiuka Miongozo ya Jumuiya ya YouTube’
YouTube ya Diamond imefutwa ikiwa na zaidi ya Subscribers milioni 6.5 na jumla ya watazamaji Bilioni 1.5. Ilikuwa na zaidi ya video 700.
Mpaka sasa haijafahamika sababu za YouTube kufuta akaunti hiyo ya YouTube ya Diamond Platnumz.
Wikiendi iliyopita akaunti ya Youtube ya Diamond Platnumz ilidukuliwa na kupandishwa maudhui ya kampuni ya magari TESLA inayomilikiwa na tajiri Elon Musk ambaye pia aliingia LIVE kwenye channel hiyo.