Hatimaye youtube channel ya mwanamuziki wa Bongofleva Diamond Platnumz imerejea tena hewani katika mtandao wa youtube baada ya kufutwa na mtandao huo.
Channel hiyo ambayo ina siku mbili tangu idukuliwe (hacked), mapema aprili 25 ilikuwa imeondolewa na youtube (terminated) kufuatia kukiuka masharti na kuvunja sheria zilizowekwa na youtube.
Baada ya Akaunti yake ya Youtube kurejeshwa, Diamond platnumz amewashukuru wote walio hakikisha Akaunti hiyo inarudi hewani na kuwataka mashabiki zake kuendelea Kuitazama video yake mpya Wonder Ambayo imerudi kwenye Trending namba 1 youtube kwa kuandika “Thank you my Beloved my Youtube channel is back, Enjoy my brand new video #WONDER ”
Akaunti hiyo imerudi kama ilivyokuwa hapo awali hakuna mabadiliko yoyote ikiwa na zaidi ya Subscribers milioni 6.5 na jumla ya watazamaji Bilioni 1.5. Ilikuwa na zaidi ya video 700.