Mwanamuziki maarufu nchini Akothee ameachia rasmi Album yake mpya inayokwenda kwa jina la Sibuor Madhako.
Sibuor Madhako Album ina jumla ya ngoma 8 za moto ambazo amewashirikisha wakali kama Tony Nyadundo na Kamanu.
Album hiyo ina nyimbo kama Siponsa, Expensive Baby, Mpenzi, Nisimamie, Abebo, Dende Nyom, Nkoro Nditu na Mapenzi Chonyi.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa Album hiyo, Akothee amesema ameachia album hiyo kwa ajili ya kuwapa moyo waliokata tamaa maishani lakini pia kwa singles mothers wote ambao wanapambana kuwalea wanao bila usaidizi wa mtu yeyote.
Sibuor Madhako ni Album ya kwanza kwa mtu mzima Akothee tangu aanze safari yake ya muziki na inapatikana ‘Exclusive’ kupitia mtandao wa Youtube.