You are currently viewing AKOTHEE ADOKEZA MPANGO KUFUNGA NDOA NA MPENZI WAKE MPYA

AKOTHEE ADOKEZA MPANGO KUFUNGA NDOA NA MPENZI WAKE MPYA

Mwimbaji na mjasiriamali maarufu nchini, Akothee anayafurahia sana mahusiano yake mapya na hivi karibuni huenda tukashuhudia akifunga ndoa na mpenzi wake mzungu.

Siku chache tu baada ya kumtambulisha mpenzi wake mpya, mama huyo wa watoto watano sasa amebainisha kuwa baada ya kuhangaika miaka mingi akitafuta mapenzi, hatimaye amempata mwenzi wa maisha.

“Sikujua kijiji changu kingeweza kuwa Paradiso, Mfalme alikuwa akikosekana, sasa naweza kusema maisha yangu yamekamilika na niko tayari kutulia, niko tayari kuwa mke mtiifu,” amesema Akothee.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram aliambatanisha ujumbe huo na picha inayomuonyesha akiwa amekumbatiwa na mpenzi wake mpya na kutangaza kwamba walikuwa wakielekea katika mbuga ya wanyama ya Ruma kwa ajili ya kutalii.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke