You are currently viewing AKOTHEE AFUNGUKA NAMNA TUHUMA ZA ILLUMINATI ZILIVYOATHIRI BINTI YAKE KIMASOMO.

AKOTHEE AFUNGUKA NAMNA TUHUMA ZA ILLUMINATI ZILIVYOATHIRI BINTI YAKE KIMASOMO.

Mwanamuziki asiyeishiwa na matukio kila leo Esther Akoth maarufu Akothee amefunguka sababu zilizompelekea binti yake Prudence Otieno aka Fancy Makadia kusomea shule mbali mbali nchini.

Kulingana na mwimbaji huyo Fancy alituhumiwa kuwa ni mshirika dhehebu la kishetani la illuminati akiwa shule ya upili ya wasichana ya Ulanda jambo ambalo lilimlazimu kumhamisha kwenye shule ghali zaidi nchini Kenya, ⁣Braeburn Group of International Schools.

Hitmaker huyo wa ngoma ya Abebo amesema tuhuma hizo zilimuathiri binti yake kisaikolajia kiasi cha kutofanya vizuri kimasomo kwani kila mara alihisi kutengwa na wanafunzi wenzake.

Hata hivyo amesema anashukuru Mungu binti yake Prudence alikamilisha masomo yake ya kidato cha nne katika shule ya Braeburn Group of International Schools na akajiunga na chuo kikuu nchini Ufaransa kusomea shahada ya masuala ya utalii na usimamizi.

Kwa sasa, Makadia yupo nchini France ambako yupo mbioni kukamilisha mtihani wake wa mwisho wiki hii ambao utatoa nafasi kwake kukamilisha masomo yake.

Mei mwaka wa 2019 Akothee alidai kuwa alimpeleka binti yake kwenye moja ya chuo kikuu ghali zaidi huko Paris, Ufaransa ambapo alienda mbali zaidi na kufichua kwamba alilipa takriban shilllingi millioni 2.2 za Kenya baada ya binti yake kujiunga na chuo hicho.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke