You are currently viewing AKOTHEE AJIBU SHTUMA ZA KUDHARAU KAZI YA MWANAMITINDO WA UREMBO NCHINI DENNIS KARURI

AKOTHEE AJIBU SHTUMA ZA KUDHARAU KAZI YA MWANAMITINDO WA UREMBO NCHINI DENNIS KARURI

Msaniii nyota nchini Akothee amemjibu mwanamitindo wa urembo nchini Dennis Karuri aliyedai kuwa msanii huyo ndiye mteja mkorofi zaidi kuwahi kumhudumia tangu aanza kujishughulisha na maswala ya urembo.

Kupitia ukurasa wake wa instagram Akothee amesema hana muda kupishana na watu wanaotafuta kiki wakitumia jina lake kwani nguvu zake zote amezielekeza kwenye ishu ya kuiweka afya yake sawa ikizingatiwa kuwa hajakuwa sawa kiafya siku za hivi karibuni.

Hitmaker huyo wa “Sweet Love” amewataka waache kumhusisha kwenye shughuli zao kwani amechoshwa kuzushiwa tuhuma za uongo ambazo amesema huenda ndizo zimempelekea kulazwa hospitali katika nyakati tofauti.

Kauli ya Akothee imekuja siku chache baada ya Dennis Karuri kwenye podcast ya Obinna kunukuliwa akisema kuwa kuna kipindi alimremba akothee lakini msanii huyo alimkatisha tamaa alipomuambia bidhaa zake za make up ni vumbi kwani zilimtoa vibaya.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke