Msanii na mfanyibiashara maarufu nchini Akothee amefunguka changamoto za kuwa mtu maarufu.
Kupitia waraka mrefu aliouchapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram Akothee amesema anajutia kuwa maarufu kwani anapata wakati mgumu sana kufurahia maisha yake ya faraghani kama watu wengine kwani mashabiki wamekuwa wakimrekodi kwa siri akiwa na familia yake maeneo ya umma.
Hitmaker huyo “Sweet Love” ameeleza kuwa kuna kipindi karibu warushiane makonde na shabiki yake mmoja ambaye alimshika akiwa anamrekodi kwa siri na familia yake.
Hata hivyo amewaomba mashabiki zake wasiwe na mazoea ya kutaka kupiga nae picha akiwa maeneo ya umma kwani amechoshwa na tabia ya watu kuingilia maisha yake.