Staa wa muziki na mfanyabiashara kutoka Kenya, mwanamama Akothee amejutia maamuzi yake ya kuwaweka watoto wake mitandaoni.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameposti chati yake ya mtandao wa WhatsApp (screenshot) na mmoja wa watoto wake ambaye anamuomba afute akaunti yake ya Instagram.
“Hili ni kosa ambalo nitaishi nikijutia, kuleta wanangu kwenye mitandao iliyojaa wachawi na uchawi kutoka kona zote za ulimwengu. Mimi nilidhani ni kitu kizuri kuonyesha maisha yangu kama njia ya kutia wengine moyo lakini wapi!” ameandika Akothee.
Akothee ambaye anafanya vizuri na wimbo wake uitwao “Nkoro Ndito” ametoa ushauri kwa wazazi wengine wasipende kuwaweke watoto wao mitandaoni huku akisema kwamba hili limesababisha aondoe uhusiano wake wa kimapenzi mitandaoni.
“Tayari ninahisi joto na itabidi nitafute njia ya kujisamehe kwa kuumiza familia yangu.” alimalizia Akothee ukupitia ukurasa wake wa Instagram.