Staa wa muziki nchini Akothee amekanusha kununuliwa gari na mpenzi wake mwenye asili ya kizungu siku chache baada ya kudai kuwa amepewa kama zawadi.
Kupitia instagram yake mama huyo wa watoto watatu amedai kuwa gari hilo lilikuwa la serikali ya kaunti.
“Gari ni ya county usikonde sweetie. Sasa 6.8 m nikitu ya kupigia kelele ,hata sijaongelea haki ,hiyo ni pesa kidogo sana kwangu” Ameandika Instagram akimjibu shabiki aliyetilia shabiki gari aliyezawadi.
Hata hivyo kauli hiyo ya Akothee imetafsiriwa kama kejeli kwa baadhi ya watu waliokuwa wanamkosoa baada ya kuweka wazi kuzawadi gari aina na mpenzi wake.
Utakumbuka katika siku za hivi karibuni Akothee amekuwa akitamba sana mtandaoni na mpenzi wake mpya tangu atangaze tena kurejea kwenye ulimwengu wa mapenzi akiwa na matarajio ya kuingia katika maisha ya ndoa amtambulishe mpenzi wake.