You are currently viewing AKOTHEE AKANUSHA KUSHIRIKI BIASHARA YA ULANGUZI WA BINADAMU

AKOTHEE AKANUSHA KUSHIRIKI BIASHARA YA ULANGUZI WA BINADAMU

Staa wa muziki nchini Akothee amekanusha vikali tuhuma za kujihusisha na biashara ya ulanguzi wa binadamu.

Hii ni baada ya walimwengu kwenye mitandao kuibua madai kuwa anamiliki kampuni inayosajili watoto wa kike nchini na kisha kuwatafutia kazi kwenye nchi za miliki ya kiarabu.

Kupitia mfululizo wa Instastory mama huyo wa watoto 5 amepuzilia mbali madai hayo huku akiwataka wanaotilia shaka utajiri wake kufanya utafiti kwanza kabla ya kuzungumzia vibaya.

Hitmaker huyo wa “Abebo” amewakejeli wanaodai kuwa utajiri wake umetokana na biashara ya ulanguzi wa binadamu, kwa kusema kuwa wamtumie vyombo vya usalama zimtie nguvuni badala ya kupiga kelele mtandaoni..

“Send DCI to come and arrest me. Aacha kupiga kelele social media. Yes, you are very right, there is no money in music,” Ameandika.

Kauli ya Akothee imekuja mara baada ya wakenya kuzua mjadala mzito kwenye mitandao ya kijamii kufuatia visa vya wasichana kudhulumiwa na waajiri wao kuongezeka katika nchini za kiarabu.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke