Msanii Akothee ameshindwa kuficha hisia zake baada ya mchekeshaji Dr. Ofweneka kumtaka alipe shillingi millioni 1.4 kama anahitaji huduma yake kama mshereheshaji kwenye hafla ya harusi yake.
Kupitia ukurasa wake wa instagram Akothee amesema mchekeshaji huyo ambaye ni rafiki yake wa karibu amedai kiasi hicho cha pesa kwa sababu anaolewa na mzungu.
Mwanamama huyo ameenda mbali zaidi na kujigamba kuwa hakuna mwanaume wa Kenya ambaye angemtosheleza kimapenzi ndio maana alikimbilia penzi la mzungu.
Hata hivyo wakenya wameonekana kumuunga mkono ofweneka kwa hatua ya kumlipisha akothee pesa nyingi wakisema mwimbaji huyo anastahili kutoa kiasi hicho cha pesa kwa kuwa ni tajiri.
Kauli ya akothee wakati huu yupo mbioni kufunga ndoa na mpenzi wake mzungu ambaye alimtambulisha juzi kati na tayari amewataka waandaji wa harusi watume maombi ya kusimamia shughuli yake ya harusi yake.