Nyota wa muziki nchini Akothee amempa somo mchekeshaji maarufu nchini Eric Omondi.
Hii ni baada ya mchekeshaji huyo kukataa kutoa mahitaji ya msingi kwa mtoto wake aliyempata na Mwanahabari Jackline Maribe hadi pale watakapofanya vipimo vya DNA.
Kupitia ukurasa wa Instagram Akothee amemtaka Eric Omondi amshughulikie mtoto wake huyo badala ya kushinikiza mtoto wao huyo afanyiwe vipimo vya DNA kwani ni kupoteza muda tu.
Mwanamama huyo wa watoto sita ameenda mbali zaidi na kusema kwamba kuna kipindi alijipata kwenye hali ya kumtaka baba ya watoto wake afanye vipimo vya DNA ili awahudumie watoto wao lakini mwisho wa siku alijipata kwenye hali kujiabisha.
Kauli ya Akothee imekuja mara baada ya Eric Omondi kujibu mapigo ya baby mama wake Jackline Maribe ambaye juzi kati alitumia mitandao yake ya kijamii kudai kwamba mchekeshaji huyo amemtekeleza mtoto wake.