You are currently viewing Akothee amsamehe mdogo wake Cebbie Koks, ataka vyombo vya habari kutoingilia ugomvi wao

Akothee amsamehe mdogo wake Cebbie Koks, ataka vyombo vya habari kutoingilia ugomvi wao

Mwanamuziki Akothee amekiri hadharani kumsamehe mdogo wake Cebbie Koks Nyasengo siku moja baada ya kudai kuwa dada yake huyo amekuwa kizingiti kikubwa kwake kufanikisha ndoa yake na mchumba wake mwenye asili ya kizungu.

Kupitia waraka mrefu aliouandika Instagram amesema licha ya kuwa mdogo wake cebbie alimtakia maneno yaliyomvunja moyo kipindi cha nyuma ameamua kumsamehe huku akisisitiza kuwa anamtabiri mema katika maisha haswa wakati huu yupo mbioni kuingia kwenye maisha ya ndoa.

Kwenye andiko lake hilo mwanamama huyo wa watoto watano amewataka wanablogu pamoja na vyombo vya habari kukoma kufufua ugomvi wao na badala yake waipe familia yake nafasi ya kutatua tofauti zao bila muingilio wowote.

Utakumbuka mapema wiki hii Akothee alifichua kuwa familia yake imekuwa kizingiti kwake kwenye mchakato wa kuiandaa harusi yake na mpenzi wake mwenye asi ya kizungu na kumtaka ahairishe shughuli hiyo kwa ajili ya kutoa nafasi kwa mdogo wake kukamilisha harusi yake mwaka huu.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke