You are currently viewing AKOTHEE AVILAUMU VYOMBO VYA HABARI NA SERIKALI KWA MASAIBU YANAYOKUMBA MUZIKI WA KENYA

AKOTHEE AVILAUMU VYOMBO VYA HABARI NA SERIKALI KWA MASAIBU YANAYOKUMBA MUZIKI WA KENYA

Nyota wa muziki Akothee amedai kwamba wasanii wa Kenya hawapati support ya kutosha kutoka kwa serikali na vyombo vya habari.

Akothee ambaye anafanya vizuri na wimbo wake mpya uitwao “Kula Ngoma” amesema vyombo vya habari nchini vimewapa wasanii wa mataifa mengine kipau mbele kuliko wasanii wa Kenya kwa kuzipiga nyimbo zao kila mara.

Ameenda zaidi na kusema ni jambo la kusikitisha kuona wasanii wa kigeni wanalipwa pesa nyingi kutumbuiza nchini huku wasanii wa Kenya wakiwekwa pembeni.

Kauli ya Akothee inakuja wakati mchekeshaji Eric Omondi ameanzisha mjadala wa kutaka muziki wa kenya upewe kipau mbele kwenye vyombo vya habari.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke