Msanii na mfanyabiashara maarufu nchini Akothee amechukizwa na kitendo cha mashabiki zake kumhusisha na taarifa za wakenya wanaodhulumiwa na waajiri wao katika nchi za miliki ya kiarabu.
Kupitia Instagram yake mwanamama huyo ameandika ujumbe wenye makasiriko akiwataka walimwengu waache tabia hiyo ambayo kwa mujibu wake inamuumiza kila mara akiona habari za wakenya wenzake wakinyanyaswa ughaibuni.
Akothee hata hivyo ametoa changamoto kwa wanaomshinikiza kutatua tatizo la wakenya kudhulumiwa Saudia Arabia kumteua kwenye wadhfa wa kisiasa kwani kwa sasa hana uwezo wa kufanikisha hilo.
Kauli yake imekuja wiki mbili baada ya kudaiwa kuwa anamiliki taasisi inayowasajili wakenya kwa ajili ya kuwatafutia kazi katika miliki za kiarabu.
Madai ambayo aliyapinga vikali akisema kwamba hayana msingi wowote ambapo alienda mbali zaidi na kutoa changamoto kwa walioibua tuhuma hizo kumshtaki kwenye vyombo vya usalama ili achukuliwe hatua kali za kisheria.