Staa wa muziki nchini Esther Akoth, maarufu Akothee amewashauri mashabiki zake kujiamini kuwa wanaweza pata amani bila usaidizi wa mtu yeyote.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Hitmaker huyo wa ngoma ya Oyoyo ameshea picha yake ya mwaka wa 2018 na kusema kwamba kipindi hicho alikuwa anapitia wakati mgumu katika maisha yake.
Akothee amesema ilibidi afanye baadhi ya mabadiliko katika maisha yake kwa ajili ya kujiweka sawa kutokana na msongo wa mawazo ikiwemo kuwapiga msasa watu waliokuwa karibu naye kipindi hicho.
Hata hivyo Akothee amewataka mashabiki zake wawe wabahili na wajiweke kipau mbele katika maisha yao kwa kujijali sana.