You are currently viewing AKOTHEE AWAPA SOMO WANAUME MTANDAONI

AKOTHEE AWAPA SOMO WANAUME MTANDAONI

Staa wa muziki nchini Akothee amewataka wanaume kuacha kumtumia jumbe tamu za kimahaba kwenye mitandao kwa nia ya kumtongoza.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mama huyo wa watoto watano ameweka wazi kuwa hawezi kuanguka kwenye mtego wa mapenzi ya mitandaoni kwa kuwa anapendelea kukutana na mtu ana kwa ana.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Sweet Love” amedokeza kuwa hofu yake ya mambo ya mitandaoni imetokana na matukio ya nyuma yaliyoishia kuuvunja moyo wake.

Hata hivyo amekiri kuwa yeye ni mwathiriwa wa unafiki ulio kwenye mitandao ya kijamii kwani amewahi kukutana na watu wengi waongo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke