Rais wa singles mothers nchini Esther Akoth maarufu kama Akothee amewaonya wazazi kukoma kuwatumia watu mashuhuri kama daraja la kulea watoto wao.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Akothee ameweka wazi kuwa mastaa hawatengenezi majina au chapa zao ili kuwa mfano wa kuigwa katika jamii.
Hit maker huyo wa ‘Kula Ngoma’ ameongeza kuwa baadhi ya vijana wana tabia ya kuiga maisha ya watu maarufu bila kujua kinachoendelea nyuma ya pazia.
Lakini pia amebainisha kuwa mitindo ya maisha ya mastaa kwenye mitandao ya kijamii kumewafanya vijana wengi kuingia kwenye msongo wa mawazo.