Msanii nyota Akothee ameamua kutaja kiasi cha pesa anacholipisha kwa show zake iwapo utahitaji kufanya kazi nae.
Katika mahojiano yake hivi karibuni Akothee ametangaza kuongeza pesa anazozilipisha kwa show moja kutoka shillingi millioni 1.5 hadi 2.3 za Kenya.
Akothee ambaye anafanya vizuri na album yake mpya iitwayo Akothee the lioness amesema amechukua hatua hiyo kutokana na bidii anayoweka kila siku kwenye shughuli zake za muziki kwani amekuwa akiwekeza pesa nyingi kutoa muziki mzuri.
Katika hatua nyingine amenyoosha maelezo maelezo kuhusu kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Nelly Oaks kwa kusema kwamba aliachana na jamaa huyo mwezi disemba mwaka jana baada ya uhusiano kuingiwa na ukungu.
Akothee amesema hayo alipokuwa anawasilisha mapendekezo ya kuwasaidia wasanii kupata shows na nyimbo zao kuchezwa kwenye vyombo vya habari katika chama cha hakimiliki na muziki na hakimiliki nchini MCSK