You are currently viewing AKOTHEE AZINDUA RASMI KITABU CHAKE

AKOTHEE AZINDUA RASMI KITABU CHAKE

Mwanamuziki na mfanyibiashara maarufu nchini, Akothee amezindua rasmi kitabu chake ambacho amekipa jina la “Akothee Quotes”.

Akothee Ametumia Ukurasa Wake Wa Instagram Kuthibitisha Hilo ambapo amesema kwamba kitabu hicho kinaelezea namna ya kufanikiwa kwenye maisha katika nyanja mbalimbali.

Kwenye kitabu hicho ambacho kinapatikana kwenye maduka kadhaa ya kuuza vitabu nchini, Akothee amesimulia kuhusu maisha yake kama mtu maarufu na maisha yake binafsi.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Abebo” anajiunga na orodha ya Mastaa ambao tayari wameandika vitabu vyao kama Janet Mbugua, Lupita Nyong’o, Polycarp Otieno wa Sauti Sol, Robert Burale na Nganga.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke