You are currently viewing Akothee azua gumzo mtandaoni kwa kutangaza baby shower ya mbwa wake

Akothee azua gumzo mtandaoni kwa kutangaza baby shower ya mbwa wake

Mwimbaji Akothee amezua gumzo mtandaoni kwa kutangaza yupo mbioni kuandaa hafla ya kusherekea mbwa wake wa kike ambaye atajifungua hivi karibuni.

Kupitia ukurasa wake wa instagram Akothee amesema atafanya baby shower ya mbwa wake aitwaye Salome jumapili hiii kwenye hafla ambayo atawaalika marafiki pamoja na wanafamilia ambao kwa njia moja au nyingine wataandamana mbwa wao wa kike na kiume.

Post hii hiyo imeibua hisia mseto miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii wengi wakitilia shaka uwezo wa kufikiria wa mwanamama huyo huku wengine wakishangaza na hatua ya Akothee kutumia pesa nyingi kumwaandalia mbwa wake baby shower wakati wakenya wanakumbwa na baa la njaa.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke