Staa wa muziki nchini Akothee ametangaza kuanza kwa ziara yake ya kimuziki mwezi Julai mwaka wa 2022 Barani Ulaya na Marekani
Akothee ameipa ziara hiyo jina la Akothee World Tour ambayo itaanza Julai 2, mwaka wa 2022 huko Munich nchini Ujerumani.
Ziara hiyo inatarajiwa kupita kwenye miji mbalimbali ikiwemo Stuttgart, Ujerumani tarehe 30 Julai, na Jonkoping, Sweden Julai 30 mwaka wa 2022.
Tour hiyo pia inatarajiwa kuzunguka kwenye miji mbalimbali nchini Marekani,Dubai, Nigeria, Tanzania, Uganda, Kenya, na Afrika Kusini ila Akothee ameahidi kuweka wazi tarehe rasmi ambayo ataanza ziara yake hiyo kwenye nchi hizo.