Mwanamuziki na mfanyibiashara maarufu nchini, Akothee anatarajiwa kuzindua kitabu chake ambacho amekipa jina la “Akothee Quotes”.
Akothee Ametumia Ukurasa Wake Wa Instagram Kuthibitisha Hilo ambapo amesema kwamba kitabu hicho kinaelezea namna ya kufanikiwa kwenye maisha katika nyanja mbalimbali.
Kwenye kitabu hicho ambacho kitazinduliwa rasmi Juni 4, mwaka huu katika hoteli ya Eka Hotel, Akothee amesimulia kuhusu maisha yake kama mtu maarufu na maisha yake binafsi.
Hata hivyo ametoa wito kwa mashabiki kukaa mkao kula kununua kitabu cha Akothee Quotes huku akisema sehemu ambayo anaipenda kwenye kitabu hicho ni ile ambayo inazungumzia maisha ya malezi ya watoto.