Mkali wa muziki wa Hiphop nchini Khalighraph Jones yupo tayari kuiboresha playlist yako hivi karibuni, Kwa mujibu wa Papa Jones anasema albamu yake mpya kutoka studio “Invisible Currency” itaingia sokoni mwezi huu wa Januari.
Khalighraph Jones ametoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa instagram ambapo ameandika ” Happy New year Everybody, 2022 we elevate, now I can finally drop Invisible Currency #respecttheogs ” hii ina maana muda wowote tunaweza kuipokea albam hiyo kutoka kwa rapa huyo.
Tayari Papa Jones tayari ameachia rasmi orodha ya nyimbo zitakazopatikana kwenye album yake mpya ya ambayo ina jumla ya nyimbo 17 huku ikiwa na collabo 10 pekee.
Hitmaker huyo wa “Luku” amewapa mashavu wakali kama Alikiba, Rude Boy, Dax, Mejja, Scar, Adasa na wengine wengi.
Invisible Currency itakuwa album ya pili kwa mtu mzima Khaligraph Jones baada ya “Testimony 1990” ya mwaka 2018 iliyokuwa na jumla ya ngoma 17.