You are currently viewing ALBAMU MPYA KUTOKA KWA KHALIGRAPH JONES INVISIBLE CURRENCY KUTOKA MACHI 7

ALBAMU MPYA KUTOKA KWA KHALIGRAPH JONES INVISIBLE CURRENCY KUTOKA MACHI 7

Mkali wa muziki wa Hiphop nchini Khalighraph Jones yupo tayari kuiboresha playlist yako hivi karibuni, kwa mujibu wa Papa Jones anasema albamu yake mpya kutoka studio “Invisible Currency” itatoka rasmi mwezi huu wa Machi.

Khalighraph Jones ametoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa instagram ambapo amewataka mashabiki zake kukaa mkao wa kula kuipokea album hiyo ambayo itaingia sokoni Machi 7 mwaka wa 2022.

Tayari Papa Jones tayari ameachia rasmi orodha ya nyimbo zitakazopatikana kwenye album yake mpya ya ambayo ina jumla ya nyimbo 17 huku ikiwa na collabo 10 pekee.

Hitmaker huyo wa “Luku” amewapa mashavu wakali kama Ali kiba, Juma Jux, Rude Boy, Dax, Mejja, Scar, Adasa na wengine wengi.

Invisible Currency itakuwa album ya pili kwa mtu mzima Khaligraph Jones  baada ya “Testimony 1990” ya  mwaka 2018 iliyokuwa na jumla ya ngoma 17

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke