Msanii wa Muziki Bongo, Jux ametangaza albamu yake mpya, ‘King of Hearts’ yenye nyimbo 16 itatoka Novemba 25 mwaka.
Hii inakuwa ni albamu ya pili ya Jux kuiachia katika safari yake ya muziki baada ya ile ‘The Love Album’ iliyoachiwa mwaka 2019.
Miongoni mwa wasanii walioshirikishwa kwenye albamu hii mpya ni pamoja na Zuchu, Mbosso, Marioo na Patoranking kutokea nchini Nigeria.
Ukiachana na Jux, wasanii wengine wanaotarajia kuachia albamu mwaka huu na Rosa Ree na Marioo.