Kundi la muziki wa Bongo Fleva ‘Navy Kenzo’ wanajiandaa kurudi na ujio wa album yao mpya.
Hitmakers hao wa ngoma ya Why Now wamekuwa wakifanya vizuri kupitia digital platforms mbalimbali, na sasa tuitarajie “Dread and love album” ambayo tayari imekamilika kwa asilimia 70.
Kwa mujibu wa Nahreel Kupitia insta story, amedokeza ujio wa album hiyo kwa kuandika ujumbe unaosomeka. “Dread & Love ALBUM 70% Loading”
Hii inaenda kuwa album ya NNE kwa Navy Kenzo, baada ya Hold me back iliyotoka mwaka wa 2015, Above inna Minute mwaka ya 2017 na Story of the African Mob iliyotoka mwaka 2020.