Ni rasmi sasa, tarehe mpya ya kuachiwa kwa album ya Wizkid imetangazwa, mkali huyo ataachia album yake mpya “More Love Less Ego” Novemba 14.
Album hiyo ya Wizkid ilikuwa imepangwa itoke Ijumaa ya wiki hii lakini kufuatia msiba wa mtoto wa kiume wa mwanamuziki mwenzake Davido, Ifeanyi Adeleke (3) ambaye amefariki mapema wiki hii, Wizkid akaghairisha kutoa album hiyo. Na kudhihirisha umma kwamba hakuna uhasama kati yake na Davido, yeye pia ameguswa na msiba huo.
Album hii mpya ya Wizkid inaenda kuwa album yake ya tano baada ya “Made In Lagos” ambayo ni ya nne, ilitoka Oktoba 30, mwaka 2020.