Nyota wa muziki nchini Uganda Azawi anazidi kuchana mbuga kimataifa hii baada ya cover ya album yake mpya iitwayo “African Music” kutumika kama art work ya chati ya new york times billboard ya nchini Marekani.
Kupitia ukurasa wake wa instagram Azawi amewatarifu mashabiki zake taarifa hiyo njema kwa kushare picha ikionyesha picha yake ambayo ilikuwa imechapisha kwenye chati ya new york times square billboard huku akiwashukuru mashabiki zake ambao wamemshika mkono hadi akafikia mafanikio hayo.
Hata hivyo Azawi anakuwa msaani wa pili kutoka Uganda album yake kutumika kama cover kwenye chati hiyo kubwa ya muziki nchini marekani baada ya Eddy Kenzo.
Mafanikio hayo yanakuja siku chache baada ya Azawi kutajwa kwamba atakuwa miongoni mwa wasanii nne wataowakilisha afrika kwenye mpango wa YouTube Black Voice Music mwaka wa 2022 unaolenga kuhamasisha wasanii, waandishi wa nyimbo,na maprodyuza kote duniani kuhusu namna ya kuboresha kazi zao za sanaa.
Ikumbukwe new york times square billboard wamekuwa na utaratibu wa kutumia picha za mastaa wa muziki ambao ngoma zao zinaongoza kwa mauzo kwenye mitandao mbali mbali ya kusikiliza muziki duniani.