Rapa kutoka nchini Uganda Fik Fameica ameendelea kutikisa katika vichwa vya habari kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kwa album yake ya King Kong.
Kwa mujibu wa takwimu album ya rapa huyo King Kong imevunja rekodi na kuwa ya kwanza katika mtandao wa kusikiliza muziki wa “Apple” kwa upande wa afrika ikiipiku album ya Burna Boy, Love Denim.
Fik Fameica ametumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa instagram kuwashukuru mashabiki zake kwa upendo ambao wanazidi kumuonyesha kupitia album yake mpya huku akiahidi kuendelea kuwapa burudani zaidi.
Album ya King Kong iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Fik Fameica imeingia sokoni rasmi Oktoba 29, mwaka wa 2022 ikiwa na jumla ya mikwaju 18.