You are currently viewing ALBUM YA HARMONIZE “AFRO EAST” YAFIKISHA STREAMS MILLIONI 15 AUDIOMACK

ALBUM YA HARMONIZE “AFRO EAST” YAFIKISHA STREAMS MILLIONI 15 AUDIOMACK

Album ya msanii Harmonize,  “Afro East” imefikisha jumla ya Streams millioni 15 kwenye mtandao wa Audiomack.

Album hiyo ya kwanza kwa mtu mzima Harmonize iliachiwa rasmi Machi 14, mwaka 2020 ikiwa na jumla ya ngoma 17 za moto.

Aidha, Boss huyo wa Konde Gang mapema mwezi huu alitangaza kuachia album yake mpya na ya tatu mwezi Juni. Ikumbukwe album yake ya pili ambayo ni “High School” ilitoka Novemba 5, mwaka 2021.

Huu unakuwa ni muendelezo wa Harmonize  kuachia ngoma mfululizo bila kupoa huku namba zikiendelea kuwa nzuri pia kupitia akaunti zake za digital platforms.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke